Jumapili, 10 Machi 2013

TANZIA: kwa wana Mgulani

Usiku wa kuamkia leo, tumepatwa na matukio mawili ya kuhuzunisha ambayo ni ya kufiwa: Nkole Rutengwe amefiwa na dada yake na pia Mohamed Abdulrahman a.k.a Alra Ul Qaime (face booK) amefiwa na baba yake.

Nkole Rutengwe anatarajiwa kusafiri kesho tarehe 11/ march/2013 kwenda morogoro ambako ndiko watakakokwenda kuzika.




Mohamed Abdulrahman yeye walishasafirisha kuelekea Tanga.

Tunawashukuru wote mlioonesha ushirikiano nasi na kwa wenzetu waliofiwa na tunaamini kuwa tutaendelea kushirikiana kwa kila jambo. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA

Maoni 3 :

  1. Kwa nafasi ya pekee kabisa, nichukue fursa hii kuwapa pole wapendwa wetu kwa majanga hayo!!
    Mungu awatie nguvu na muamini kuwa wapendwa wetu waliotutangulia wapo kwenye pumziko la heri, na siku moja tutajumuika nao kwa upendo katka maisha yasiyo na mwisho.
    Wapumzike kwa amani wapendwa wetu Amen!!

    Lugano

    JibuFuta
  2. thanks kaka Luggy, usemalo ni la kweli tupu ndugu yangu

    JibuFuta
  3. Ahsanteni sana wakuu!!!mimi na familia yangu tumepoa Alhamdulillah.
    Mwenyezi Mungu awazidishie kila jema maradufu.

    JibuFuta