Jumatano, 27 Machi 2013

Serikali yajipanga kudhibiti mfumuko

Dar es Salaam, Serikali imesema itahakikisha katika mwaka wa fedha 2013/14 mfumuko wa bei, unapungua hadi kufikia asilimia 10 na hatimaye kufikia tarakimu moja.
Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mapendekezo ya mipango ya maendeleo ya taifa katika  mwaka wa fedha wa 2013/14, Tume ya Mipango, itahakikisha kuwa mfumko wa bei unazidi kupungua.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Rais, inasema katika miaka ya fedha iliyopita, mfumuko wa bei ulipungua kutoka asilimia 19.8 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 12 mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi kuhusu mwelekeo wa bajeti,  Waziri wa Fedha na Uchumi ,Profesa William Mgimwa, alisema kimsingi Serikali inajipanga ili kuhakikisha kuwa inapunguza zaidi mfumuko wa bei.
“Tunataka hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, mfumuko wa bei uanzie  asilimia 10 na baadaye kufikia tarakimu moja,” ilisema Profesa Mgimwa.
Alisema kwa sasa mfumuko katika bei za vyakula, umeshuka hadi kufikia asilimia 13.3
mwaka 2012 kutoka asilimia 25.6 na kwamba hatua hiyo, inatokana na  juhudi za Serikali za kuimarisha upatikanaji wa chakula.
Mgimwa alisema  mfumuko wa bei wa nishati, umeshuka hadi kufikia asilimia 17.8 kutoka asilimia 41.0.
Akizungumzia deni la taifa, waziri huyo  alisema  limeongezeka khadi ufikia Dola 12 bilioni za Marekani mwaka 2012 kutoka Dola  11 bilioni mwaka juzi.
Kwa mujibu wa Profesa Mgimwa, Dola 10 bilioni katika fedha hozi nio deni la umma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni