Jumatano, 27 Machi 2013

Cheti alichotumia Mulugo cha Mhadhiri wa Mkwawa

Dar es Salaam. Imebainika kuwa mmoja wa watu ambao Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (pichani)anadaiwa kutumia jina lake kutafuta kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari ya Southern mkoani Mbeya ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (Muce), kilichopo mkoani Iringa.


Mhadhiri huyo ni Dick Aron Mulungu ambaye alisoma na Mulugo katika Shule ya Sekondari ya Songea Wavulana kati ya 1994 na 1996 na alijiunga na shule hiyo baada ya kuhitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kafule, ambayo iko mkoani Mbeya.


Taarifa zinaonyesha kuwa Mulungu alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata Shahada ya kwanza katika Elimu (BA Education) 2001 na baadaye alisoma na kupata Shahada ya Uzamili (MA Development studies ) 2007.


Alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi, mahojiano yalikuwa hivi:
Mwandishi: Hallow…(mwandishi akajitambulisha)
Mulungu: Sawa, unasemaje?
Mwanishi: Nazungumza na Dick Mulungu?


Mulungu: Ndiyo mimi.
Mwandishi: Hivi unamfahamu mtu anayeitwa Hamimu Agustino?
Mulungu: Aah… hivi ulisema unaitwa nani?
Mwandishi: Si nimeshajitambulisha jina na ofisi ninayotoka?
Mulungu: Nipigie kesho naona hapa kuna kelele.


Mwandishi: Mbona nakusikia vizuri tu?
Mulungu: Nipigie baada ya nusu saa basi.
Baada ya nusu saa…….
Mwandishi: Haloo… naona nusu saa imekwisha, uko tayari kuzungumza?
Mulungu: Huyo simfahamu.
Mwandishi: Kwani wewe si ulisoma Songea Boys?


Mulungu: Ndiyo
Mwandishi: Kwa hiyo humkumbuki mtu aliyekuwa akitumia jina hilo?
Mulungu: Huyo mtu namkumbuka ndiyo.
Mwandishi: Kwa sasa yuko wapi?
Mulungu: Siwezi kujua, si unajua tumesoma siku nyingi sasa huwezi kujua mtu amekwenda wapi… ni siku nyingi mno.
Mwandishi: Ahsante.

Chuo Kikuu na siasa
Taarifa zinaonyesha kuwa Waziri Mulugo alijiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania 2002 akitumia majina ya Philipo Hamimu Augustino na alisomea Shahada ya Sanaa katika Elimu (BA. Ed). Namba yake ya usajili chuoni hapo ni 08652/T.02.
Alipokuwa akiendelea na kazi ya ualimu Mulugo alianza harakati za kisiasa na ndipo alipoamua kwenda kugombea ubunge katika majimbo ya wilaya ya Chunya.


Kada wa chama cha NCCR Mageuzi wilayani Chunya, Nyawili Kalenda aliyejitambulisha kama mlezi wa siasa wa Waziri huyo alisema walifahamiana naye 2004 wakati Mulugo na rafiki yake walipokwenda kumtaka ushauri wa kugombea ubunge katika jimbo la Songwe.


Katika nakala za wasifu wake zinaonyesha kuwa 2008 alishika nafasi ndani ya CCM ambazo ni pamoja na mjumbe wa baraza la jumuiya ya wazazi wilaya ya Chunya, Katibu wa Elimu, Uchumi, Malezi na mazingira wa jumuiya ya wilaya hiyo na mjumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Mbeya.

Kauli yake
Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule. “Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo.


Licha ya kukiri kurudia darasa la saba, Waziri Mulugo alisema jina la Hamimu amekuwa akilitumia katika elimu tangu awali na kwamba hakuvunja sheria kufanya hivyo.


“Jina la Hamim ni la nyumbani Philipo ni jina langu la ubatizo, nadhani haya ni mambo ya kawaida na kweli nilipokuwa shule watu walikuwa wananifahamu kama Hamimu pia Philipo ni jina langu la ubatizo na kumbuka tukifika chuo huwa tunatumia jina la baba.


“Na pia ni kweli nilirudia shule kwa sababu wakati ule wa Mwalimu Nyerere na Mwinyi (Ali Hassan), sheria ilikuwa inaruhusu maana wanafunzi walikuwa wachache mno, fikiria katika darasa letu la saba tulimaliza watu saba tu. Baadaye sheria hiyo ilibadilishwa,” aliongeza.

Kuhusu jina la Dick Mulungu, alikiri kumfahamu mtu huyo na kwamba walisoma wote shule ya Sekondari ya Songea Boys. Hata hivyo, alipinga kutumia vyeti vyake.“Ni kweli Dick Mulungu tulisoma wote Songea Boys. Lakini hili jina la Mulungu ni jina letu la ukoo. Babu yangu alikuwa akiitwa Filipo Milambo Mulungu, kwa hiyo niliendelea kulitumia hivyo hivyo na hata jina la Mulugo ni letu pia,” alisema.

Simulizi ya muuguzi alivyofanyiwa unyama Kibaha

Tarehe 26 ya mwezi wa 12, mwaka 2011, pengine ni siku isiyoweza kusahaulika katika kumbukumbu za msichana mrembo Mishaly Sumary.
Ni siku ambayo binti  huyu wa miaka 26 tu, alipokutana na mkasa uliomsababisha kupooza  mwili wake wote.
Ilikuwa ni siku moja tu baada ya sikukuu ya Krismas.Mishaly, alikuwa akitoka kazini kwake yeye ni muuguzi katika Hospitali ya Dk Joseph Bakes, Kibaha.
Saa moja na nusu jioni, alipigiwa simu na dada wa rafiki yake, ambaye alikuwa akihitaji ushauri.
Walikubaliana wakutane katika eneo la lango Kuu Kibaha. Mazungumzo yao yalipomalizika, Mishaly, alitaka kuchukua usafiri wa bodaboda, ili umuwahishe nyumbani kwake. Lakini rafiki  yake alimshauri atembee kwa miguu kwa kuwa usiku haukuwa mwingi.
Mishaly, aliukubali ushauri ule na akaanza kuchepuka akielekea nyumbani kwake.
Dakika kumi tu, baada ya kuagana na rafiki yake, Mishaly alisikia kishindo cha watu nyuma yake.
Ghafla aliwaona wanaume wawili  wakimwendea kwa kasi. Walimkaba, mmoja akimshika miguu na mwingine akiikamata shingo yake.
“Nilijaribu kupiga kelele, lakini mmoja wao alinikaba shingoni, nilijitahidi kupigana nao lakini haikuwa kazi rahisi,” anasema Mishaly
Wanaume wale walimwambia: “Sali sala yako ya mwisho”
Lakini Mishaly aliendelea kujitetea kwa kurusha miguu.
Walitaka kumrusha katika kisima cha Dawasco kilichopo karibu na eneo hilo, lakini wakaachana na wazo hilo.
Walipoona anajitetea kwa nguvu, mmoja akaikunja mikono yake miwili kwa nyuma…akaweka goti katikati ya mgongo… na kumvunja mithili ya mtu avunjavyo muwa.

“Nilipiga kelele kwa maumivu makali niliyoyapata, nikasikia watu wanakimbilia katika lile eneo, nikawasikia wale wanaume wakisema, maliza kazi tusiuze gazeti,” anasimulia Mishaly

Katika kumalizia uhalifu huo, mmoja wa  wanaume wale alichukua chuma bapa chenye urefu wa mkono wa mtu mzima, na kumpiga nacho mdomoni.

Kwa kitendo kile, Mishaly alivunjika meno mawili, na kupasuka mdomo sehemu ya chini.

Wakati huo huo, mwanaume mwingine aliishika shingo ya binti huyo na kuizungusha mithili ya dereva akataye kona kwa nguvu.

“Watu walianza kujaa katika lile eneo,  aliyenivunja shingo akakimbia, lakini nikamshika shati  yule wa mbele aliyenipiga na chuma,” anasema

Katika kujaribu kukimbia, kijana aliyeshikwa shati alimng’ata Mishaly mdomoni. Alimng’ata kwa nguvu kiasi kwamba meno yalipenyeza ndani ya mdomo.

Baada ya kumng’ata alivua shati lake na kukimbilia katika vichaka.

Mishaly alipelekwa polisi na wasamaria wema, hata hivyo ilimchukua saa nne kuandikiwa PF3, na aliendelea kuteseka na maumivu makali.

“Nilikimbizwa katika hospitali ya Tumbi, lakini hali iliendelea kuwa mbaya na nikapewa rufaa ya kwenda Muhimbili. Hata hivyo nilikutana na mgomo mkali wa madaktari,” anasema

 Ilimchukua muda kupata huduma stahiki, na akiwa hapo Muhimbili, mwili wake wote ukaingia ganzi.

 “Sikuwa na hisia zozote kuanzia mikononi hadi miguuni…sikuweza kufanya chochote, kichwa changu tu ndicho kilikuwa na ufahamu” anasema
Alihamishwa tena na kupelekwa katika hospitali ya Dk Bakes ambapo ndipo kazini kwake. Hapo Mishaly alipata matibabu mazuri, anakiri kuwa mwajiri wake alitumia ujuzi wake kumtibu pale alipoweza.

Picha ya X-ray ilionyesha kuwa pingili tatu za uti wa mgongo wa Mishaly zimekatika. Lakini pia, nyonga yake ilikuwa imeharibiwa vibaya.

 Aidha, shingo yake lilikuwa limeharibiwa na kuvunjika vunjika.

“Nilitakiwa kwenda Muhimbili kwa wataalamu wa mishipa lakini hata hivyo wakasema hawataweza kunifanyia upasuaji kwa sababu mishipa yangu ya damu imekufa. Wanachoweza kunisaidia ni mazoezi tu,” anasema

Mishaly anatakiwa kufanyiwa upasuaji nchini India, ili arejee tena katika uzima wake wa awali.

Akiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto tisa, Mishaly hana ndugu hapa jijini na hivi sasa amepewa hifadhi katika familia ya mzee wa kanisa lake.

“Familia yangu ni ya kimaskini, mama yangu ni mgonjwa yu taabani, na sijui nitapata wapi fedha za kutibiwa nje ya nchi,” anasema

 Hata fedha za kwenda kufanya mazoezi Muhimbili, Mishaly huchangiwa na waumini wenzake.

 Mishaly, binti mdogo ambaye bado mchango wake unahitajika kwa taifa, hajiwezi kwa lolote. Ni wa kubebwa, kufuliwa, na muda wake mwingi anautumia akiwa kitandani.

 Baada ya mazungumzo yetu, Mishaly anamaliza na ujumbe huu:

“Namuomba Mungu aninyanyue hapa kitandani, na iwapo haitampendeza mimi kunyanyuka, basi …namsihi niwepo katika ufalme wake”.

Familia ya Mzee Nyange inayomtunza Mishaly haikutaka kuzungumza lolote.
 

Serikali yajipanga kudhibiti mfumuko

Dar es Salaam, Serikali imesema itahakikisha katika mwaka wa fedha 2013/14 mfumuko wa bei, unapungua hadi kufikia asilimia 10 na hatimaye kufikia tarakimu moja.
Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mapendekezo ya mipango ya maendeleo ya taifa katika  mwaka wa fedha wa 2013/14, Tume ya Mipango, itahakikisha kuwa mfumko wa bei unazidi kupungua.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Rais, inasema katika miaka ya fedha iliyopita, mfumuko wa bei ulipungua kutoka asilimia 19.8 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 12 mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi kuhusu mwelekeo wa bajeti,  Waziri wa Fedha na Uchumi ,Profesa William Mgimwa, alisema kimsingi Serikali inajipanga ili kuhakikisha kuwa inapunguza zaidi mfumuko wa bei.
“Tunataka hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, mfumuko wa bei uanzie  asilimia 10 na baadaye kufikia tarakimu moja,” ilisema Profesa Mgimwa.
Alisema kwa sasa mfumuko katika bei za vyakula, umeshuka hadi kufikia asilimia 13.3
mwaka 2012 kutoka asilimia 25.6 na kwamba hatua hiyo, inatokana na  juhudi za Serikali za kuimarisha upatikanaji wa chakula.
Mgimwa alisema  mfumuko wa bei wa nishati, umeshuka hadi kufikia asilimia 17.8 kutoka asilimia 41.0.
Akizungumzia deni la taifa, waziri huyo  alisema  limeongezeka khadi ufikia Dola 12 bilioni za Marekani mwaka 2012 kutoka Dola  11 bilioni mwaka juzi.
Kwa mujibu wa Profesa Mgimwa, Dola 10 bilioni katika fedha hozi nio deni la umma.

KIKAO CHA WANA-MGULANI NI 30/3/2013

Wajumbe wa Mgualni 99 organization, kikao chetu kitakuwa tarehe 30/3/2013. Wajumbe wote halali mnatakiwa kuhudhuria kikao chetu hicho ambacho kiutaratibu ni kikao chetu cha tatu kikatiba. Kikao chetu kitakuwa na mambo kadhaa ya kujadiliana ili kuweza kufikia malengo kusudiwa

Alhamisi, 21 Machi 2013

Wanafunzi washinda danguroni Dar

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Yasinta Assey akionyesha baadhi ya nguo na viatu vya wanafunzi vilivyokutwa katika eneo linalodaiwa kuwa danguro linalotumiwa na wanafunzi wa shule hiyo, jana.

MWANZA,MWANZA

Jumamosi, 16 Machi 2013

KIKAO CHA LEO TAREHE 16/MARCH/2013

 Baadhi ya wanachama wakiwa wanawasubiri wanachama wengine wafike ili kikao kianze
hapo kuna jackson Mathew, John Nkungu, Joseph Massamu na Suzanna Kanju
 picha hii: Uhoto; Suzanna Kanju, Elton Mnunga, Jackson Mathew na Jihn Nkungu
 Kadri mudas ulivyoukuwa unakwenda ndivyo wajumbe walikuwa wanaongezeka
hawa ni :kushoto ni Nkole Rutengwe, Imani Kifukwe na John Nkungu wakiwa wasalimiana habari za siku nyingi
 KATIKATI NI" Said Jongo ndio amewasili katika kikao
Bado ni maongezi tu, kuhusu mambo mbalimbali kabla ya kikao

Ijumaa, 15 Machi 2013

MWENDELEZO WA MCHAKATO WILAYANI

 Picha hii ni eneo la Manispaa ya Temeke ambapo mcghakato wa Usajili umekuwa ukifanyika kwa siku kadhaa
 M/hazina akiwa ametoka wilayani kufuatilia masuala ya mchakato wa usajili.
M/hazina akiwa pamoja na Katibu katika kuhaikisha mambo yanaenda vizuri. wameutana hapo baada ya kuwa wamepitia maeneo mbalimbali ili kufanisha suala zima la usajili wa MGULANI 99 ORGANIZATION

MCHAKATO WA UAJILI WA ORGANIZATION

 Picha hiyo inamuonesha M/hazina akiwa katika mchakato wa kufuatilia masuala ya TIN no. na kodi ambazo tutawajibika kuzilipa pindi tu mambo ya kupatiwa TIN namba yatakapokamilika muda si mrefu. Bwana Massamu anastahili kupongezwa kwa kazi nzuri ya kujumika na viongozi wenzake wa Organization kwa jinsi anavyojitolea muda na jitihada zake katika kuhakikisha kuwa mambo yanaenda sawa
picha hii ni Joseph Massamu - M/HAZINA, Elton Mnunga- KATIBU na John Nkungu-MWENYEKITI. viongozi wa Orginization wakiwa wamepumzika ili pia kupata wasaha wa kubadilishana mawazo ya nini kifanyike baada ya mchakato wa siku hiyo. Siku hii ilikuwa na mambo mengi sana lakini hakuna lenye mwanzo linalokosa kuwa na mwisho

Jumanne, 12 Machi 2013

Aibu,vyoo vya shule karne ya 21

Kwa ufupi
Tafiti zabainisha shule nyingi nchini zina vyoo duni sana  ukilinganisha na mataifa mengine Afrika Mashariki. Wasomi wasema vyoo visivyofaa huchangia maendeleo mabaya kwa watoto wa kike hasa waliovunja ungo, kwa vile hushindwa kujisitiri vizuri wanapokuwa hedhi, hivyo kusababisha baadhi yao kutokwenda shule.
Wanafunzi wa kike hulazimika kuomba huduma za kujisaidia kwenye vyoo vya karibu na shule, huko baadhi yao wanabakwa au kufanyiwa ukatili mwingine wowote

HII NI NYINGINE TENA YA 1999

Haya tena ndugu zangu na hebu tuwakumbuke na hawa wafuatao;

KUSHOTO KUELEKEA MSTARI WA NYUMA: Elton mnunga, Oscar Leonard, Mustafa Shaibu, Ahobokile Mwandiga, anayefuata jina limenitoka lakini alikuwa ni mtu wa vituko na komedi sana,kama utamkumbuka jina hebu niambie na mimi nimkumbuke, anayefuata ni David Kasanja, Said Adamu, Clarence John na nyuma yake pia nimemsahau dah sijui inakuwaje lakini ndo hivyo sababu ya muda ni mrefu umepita

MSTARI WA MBELE: Mathew Mgwabati, Abdul Sultan, Nelson Rwezaura na Imani Kifukwe

Picha hii pia ni baadaya mtihani wa darasa la saba mwaka 1999

MWAKA 1999- MARA TU BAADA YA NECTA



Siku hii ni siku ambayo tulimaliza mtihani wa darasa la saba, naamini baadhi yenu mtakuwa mnakumbuka vizuri sana siku hii, kwa sababu ilikuwa na matukio tofauti tofauti.

UTAMBULISHO
Kama utakuwa umesahau kuhusu majina ya watu hawa na hebu nikukumbushe

KUANZIA KUSHOTO WALIOSIMAMA: Nkole Rutengwe, Laurian William, Daniel Manege, Baba Tojo au kwa jina rasmi ni Thobias Jonas, ni kama anachana mistari vile huyo ni Lugano Nissa, pembeni yake kijana anayeonekana kama mtulivu vile,huyo ni Mathew Mgwabati, pembeni yake ni Eva Greyson na mwisho ni Elton Mnunga

KUANZIA KUSHOTO WALIOCHUCHUMAA: Elias Mwanyika a.k.a Kanali vijoka au Madodo. aliyeinamisha kichwa chini ni Mustafa shaibu au Chafaka mzee wa kukuzimia sigara ya macho kama utamzingua, pembeni yake ni Colman Peter Kadili. Binti aliyeshikwa bega ni Tabitha Mfikwa na mwisho kabisa ni Beda Peter a.k.a Rick Rose baada ya kuwa mtu mzima ndo anajiita jina hilo.

Niambie unakumbukumbu gani nyingine, hebu weka picha au toa maoni yako hapo

Jumapili, 10 Machi 2013

WAJUMBE WALIOSHIRIKI KIKAO CHA TAREHE 19, JANUARI, 2013


KUTOKA KUSHOTO: Beda Peter, Daniel Athony, Jackon Mathew, Yahaya Bozi Kibambe,Mrock abisai na Adolf Miyungua

Hao ni baadhi ya waanzilishi wa Mgulani 99 Organization

TANZIA: kwa wana Mgulani

Usiku wa kuamkia leo, tumepatwa na matukio mawili ya kuhuzunisha ambayo ni ya kufiwa: Nkole Rutengwe amefiwa na dada yake na pia Mohamed Abdulrahman a.k.a Alra Ul Qaime (face booK) amefiwa na baba yake.

Nkole Rutengwe anatarajiwa kusafiri kesho tarehe 11/ march/2013 kwenda morogoro ambako ndiko watakakokwenda kuzika.




Mohamed Abdulrahman yeye walishasafirisha kuelekea Tanga.

Tunawashukuru wote mlioonesha ushirikiano nasi na kwa wenzetu waliofiwa na tunaamini kuwa tutaendelea kushirikiana kwa kila jambo. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA

Jumatano, 6 Machi 2013

ATHARI ZA MAFURIKO

akina nani ni wahanga wa mafuriko?

Mbatia ajitoa Tume ya kuchunguza kushuka elimu


Kwa ufupi
Mbatia ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wajumbe wa tume hiyo yenye wajumbe 15, alisema kamwe hatoweza  kufanya kazi yake kwa uhuru kwa sababu  ni Mbunge wa kuteuliwa, kamati hiyo imeundwa na serikali hivyo lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.

MGULANI ENZI HIZO, WAKUMBUKA?


RAIS WA VENEZUELA AFARIKI DUNIA

Kwa ufupi
Amefariki akiwa na umri wa miaka 58, Makamu wa Rais Nicola Maduro amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Awali ilielezwa kuwa Rais Chavez alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kansa

Jumanne, 5 Machi 2013

WALIMU WAPYA KIGOMA WAANGUA KILIO

katika hali isiyo ya kawaida walimu wapya waliopangiwa Kigoma wameangua kilio  baada ya kuona wanapelekwa katika maeneo wasiyo tegemea, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma emikri hali hiyo nma kuwaoma walimu wasikate tamaa, lakini je ni kweli mazingira ya walimu ni mazuri kiasi cha kuwafanya kupenda kazi yao?

WATOTO WA MTAANI WANA HATARI KUBWA YA KUINGIA KATIKA UVUTAJI WA DAWA ZA JUKEVYA

Tuisadie jamii katikam kuepukana na haya, tuanze sasa kwa kujitolea na tukiwaomba wadau wengine watupe support katika kufanikisaha tunayoyapanga

UKITOA AIBU UTAFANIKIWA



NINI KINAWAFANYA WANAFUNZI KUPOTEZA MWAMKO WA ELIMU?


 Mwanafunzi anayeshindwa kuandika hata kidogo katika mtihani na anaamua kuchora picha zisizoelweka, tatizo ni nini hasa? hebu tupate maoni ya nini kifanyike kuinua ari ya vijana kupenda elimu?

HERI PUNDA AFE LAKINI MZIGO UFIKE


KUNA USALAMA?


PICHA 1 KUSHOTO: mzazi na watoto wake wakivuka daraja hatarishi. PICHA 2 KULIA: Mwendesha pikipiki akivuka daraja hatarishi kwa shida . PICHA 3 CHINI: Wasichana wakivuka daraja hatarishi.


AJALI KAZINI

Usalama kazini ni muhimu

JE TUTAFIKA?


Tazama, huyu anajitafutia riziki, je yupo salama?




TUNAISAIDIAJE JAMII YETU KUTOKA KATIKA UMASKINI?


Wazazi wetu hususani wale wa vijijini wamekuwa na maisha duni ambayo hayatoi mwanga wa kesho yao inakuwaje, hali hii ya uduni ndiyo inayopelekea vijana wengi kukimbilia mijini wakidhani ndiko kwenye maisha rahisi lakini kumbe ni tofauti na uhalisia wake. Vijana wenzangu hebu tatafakari haya kwa kina na kwenda kuwatembelea vijana wenzetu wa vijini ambao kwa kiasi kikubwa wamekosa motisha ya maisha chanya. Tuwatembelee na kuwapa changamoto kuwa wao ndio tegemeo pekee la kuleta mabadiliko katika maeneo yao na pia kuwapa mbinu za kujiinua kimaisha.. Toa moani yao ni namna ya kuweza kuwafikia vijana wenzetu





TAZAMA WADOGO ZETU WANAVYOPATA TABU YA USAFIRI



Jamii yetu inapaswa kuangalia mambo kama haya ili kusaidia vijana kupata elimu bora, mazingira hatarisha kama haya yanapelekea wanafunzi kutoona umuhimu wa elimu na wengine hushindwa kufikia malengo au ndoto zao. Mazingira ya elimu yakiboreshwa hakuna atakaye iogopa elimu. Tuisaidie jamii katika kupambana 



Hiyo ndo Logo Ya Mgulani 99 Organization wadau,

Ijumaa, 1 Machi 2013

The Only Place where you Meet your Old school Friends and Share the future

 KUUNDWA KWA ASASI YA  MGULANI 99 ORGANIZATION

Vijana waliohitimu shule ya msingi Mgulani walikutana tarehe 19/ januari/2013 na kuamua kuunda asasi itakayokuwa na malengo ya kuisaidia jamii katika masuala mbalimbali hususani yale mtambuka kama vile athari za mabadiliko ya hali yahewa, ujinga na umaskini kwa njia ya kujitolea ( voluntarily)