Jumanne, 16 Aprili 2013

mlipuko boston

mlipuko mkubwa umetokea Nchini Boston ambapo watu 170 wamejeruhiwa katika mlipuko huo

Ijumaa, 5 Aprili 2013

MATUKIO SIKU YA KIKAO CHA TAREHE 30/3/2013


Enzi za Abiko Hall, hapo tupo tunajaribu kukumbushia


Mgulani ilivyo hivi sasa: Darasa la Saba A na B yanaonekana, kushoto kwake ndiyo  kuna Abiko Hall



 

Jumanne, 2 Aprili 2013

KIKAKO CHA TAREHE 30/3/2013

WALIOSHIRIKI NI HAO

Siku hii tulipata wajumbe wengi ambao walikuwa charming sana: nikianzia kushoto waliosimama nikwamba tuna : Zakayo Dominick, Andrew Mande , Shamira Shaibu, Suzanna Kanju, Mohamed Abdulrahman a.k.a Alra Ul Qaime, Lugano Nissa, Daniel Athony, Imani Kifukwe, John Nkungu, Abdul Sultan, Yahaya a.k.a Yaki Bozi na Nkole Rutengwe

Waliochuchumaa kuanzia kushoto ni: Joseph Massamu, Elias Mwanyika na Victor Akyoo Ngole
siku hiii ilikuwa ni siku nzuri kwa tuliokutana

Jumatano, 27 Machi 2013

Cheti alichotumia Mulugo cha Mhadhiri wa Mkwawa

Dar es Salaam. Imebainika kuwa mmoja wa watu ambao Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (pichani)anadaiwa kutumia jina lake kutafuta kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari ya Southern mkoani Mbeya ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (Muce), kilichopo mkoani Iringa.


Mhadhiri huyo ni Dick Aron Mulungu ambaye alisoma na Mulugo katika Shule ya Sekondari ya Songea Wavulana kati ya 1994 na 1996 na alijiunga na shule hiyo baada ya kuhitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kafule, ambayo iko mkoani Mbeya.


Taarifa zinaonyesha kuwa Mulungu alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata Shahada ya kwanza katika Elimu (BA Education) 2001 na baadaye alisoma na kupata Shahada ya Uzamili (MA Development studies ) 2007.


Alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi, mahojiano yalikuwa hivi:
Mwandishi: Hallow…(mwandishi akajitambulisha)
Mulungu: Sawa, unasemaje?
Mwanishi: Nazungumza na Dick Mulungu?


Mulungu: Ndiyo mimi.
Mwandishi: Hivi unamfahamu mtu anayeitwa Hamimu Agustino?
Mulungu: Aah… hivi ulisema unaitwa nani?
Mwandishi: Si nimeshajitambulisha jina na ofisi ninayotoka?
Mulungu: Nipigie kesho naona hapa kuna kelele.


Mwandishi: Mbona nakusikia vizuri tu?
Mulungu: Nipigie baada ya nusu saa basi.
Baada ya nusu saa…….
Mwandishi: Haloo… naona nusu saa imekwisha, uko tayari kuzungumza?
Mulungu: Huyo simfahamu.
Mwandishi: Kwani wewe si ulisoma Songea Boys?


Mulungu: Ndiyo
Mwandishi: Kwa hiyo humkumbuki mtu aliyekuwa akitumia jina hilo?
Mulungu: Huyo mtu namkumbuka ndiyo.
Mwandishi: Kwa sasa yuko wapi?
Mulungu: Siwezi kujua, si unajua tumesoma siku nyingi sasa huwezi kujua mtu amekwenda wapi… ni siku nyingi mno.
Mwandishi: Ahsante.

Chuo Kikuu na siasa
Taarifa zinaonyesha kuwa Waziri Mulugo alijiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania 2002 akitumia majina ya Philipo Hamimu Augustino na alisomea Shahada ya Sanaa katika Elimu (BA. Ed). Namba yake ya usajili chuoni hapo ni 08652/T.02.
Alipokuwa akiendelea na kazi ya ualimu Mulugo alianza harakati za kisiasa na ndipo alipoamua kwenda kugombea ubunge katika majimbo ya wilaya ya Chunya.


Kada wa chama cha NCCR Mageuzi wilayani Chunya, Nyawili Kalenda aliyejitambulisha kama mlezi wa siasa wa Waziri huyo alisema walifahamiana naye 2004 wakati Mulugo na rafiki yake walipokwenda kumtaka ushauri wa kugombea ubunge katika jimbo la Songwe.


Katika nakala za wasifu wake zinaonyesha kuwa 2008 alishika nafasi ndani ya CCM ambazo ni pamoja na mjumbe wa baraza la jumuiya ya wazazi wilaya ya Chunya, Katibu wa Elimu, Uchumi, Malezi na mazingira wa jumuiya ya wilaya hiyo na mjumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Mbeya.

Kauli yake
Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule. “Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo.


Licha ya kukiri kurudia darasa la saba, Waziri Mulugo alisema jina la Hamimu amekuwa akilitumia katika elimu tangu awali na kwamba hakuvunja sheria kufanya hivyo.


“Jina la Hamim ni la nyumbani Philipo ni jina langu la ubatizo, nadhani haya ni mambo ya kawaida na kweli nilipokuwa shule watu walikuwa wananifahamu kama Hamimu pia Philipo ni jina langu la ubatizo na kumbuka tukifika chuo huwa tunatumia jina la baba.


“Na pia ni kweli nilirudia shule kwa sababu wakati ule wa Mwalimu Nyerere na Mwinyi (Ali Hassan), sheria ilikuwa inaruhusu maana wanafunzi walikuwa wachache mno, fikiria katika darasa letu la saba tulimaliza watu saba tu. Baadaye sheria hiyo ilibadilishwa,” aliongeza.

Kuhusu jina la Dick Mulungu, alikiri kumfahamu mtu huyo na kwamba walisoma wote shule ya Sekondari ya Songea Boys. Hata hivyo, alipinga kutumia vyeti vyake.“Ni kweli Dick Mulungu tulisoma wote Songea Boys. Lakini hili jina la Mulungu ni jina letu la ukoo. Babu yangu alikuwa akiitwa Filipo Milambo Mulungu, kwa hiyo niliendelea kulitumia hivyo hivyo na hata jina la Mulugo ni letu pia,” alisema.

Simulizi ya muuguzi alivyofanyiwa unyama Kibaha

Tarehe 26 ya mwezi wa 12, mwaka 2011, pengine ni siku isiyoweza kusahaulika katika kumbukumbu za msichana mrembo Mishaly Sumary.
Ni siku ambayo binti  huyu wa miaka 26 tu, alipokutana na mkasa uliomsababisha kupooza  mwili wake wote.
Ilikuwa ni siku moja tu baada ya sikukuu ya Krismas.Mishaly, alikuwa akitoka kazini kwake yeye ni muuguzi katika Hospitali ya Dk Joseph Bakes, Kibaha.
Saa moja na nusu jioni, alipigiwa simu na dada wa rafiki yake, ambaye alikuwa akihitaji ushauri.
Walikubaliana wakutane katika eneo la lango Kuu Kibaha. Mazungumzo yao yalipomalizika, Mishaly, alitaka kuchukua usafiri wa bodaboda, ili umuwahishe nyumbani kwake. Lakini rafiki  yake alimshauri atembee kwa miguu kwa kuwa usiku haukuwa mwingi.
Mishaly, aliukubali ushauri ule na akaanza kuchepuka akielekea nyumbani kwake.
Dakika kumi tu, baada ya kuagana na rafiki yake, Mishaly alisikia kishindo cha watu nyuma yake.
Ghafla aliwaona wanaume wawili  wakimwendea kwa kasi. Walimkaba, mmoja akimshika miguu na mwingine akiikamata shingo yake.
“Nilijaribu kupiga kelele, lakini mmoja wao alinikaba shingoni, nilijitahidi kupigana nao lakini haikuwa kazi rahisi,” anasema Mishaly
Wanaume wale walimwambia: “Sali sala yako ya mwisho”
Lakini Mishaly aliendelea kujitetea kwa kurusha miguu.
Walitaka kumrusha katika kisima cha Dawasco kilichopo karibu na eneo hilo, lakini wakaachana na wazo hilo.
Walipoona anajitetea kwa nguvu, mmoja akaikunja mikono yake miwili kwa nyuma…akaweka goti katikati ya mgongo… na kumvunja mithili ya mtu avunjavyo muwa.

“Nilipiga kelele kwa maumivu makali niliyoyapata, nikasikia watu wanakimbilia katika lile eneo, nikawasikia wale wanaume wakisema, maliza kazi tusiuze gazeti,” anasimulia Mishaly

Katika kumalizia uhalifu huo, mmoja wa  wanaume wale alichukua chuma bapa chenye urefu wa mkono wa mtu mzima, na kumpiga nacho mdomoni.

Kwa kitendo kile, Mishaly alivunjika meno mawili, na kupasuka mdomo sehemu ya chini.

Wakati huo huo, mwanaume mwingine aliishika shingo ya binti huyo na kuizungusha mithili ya dereva akataye kona kwa nguvu.

“Watu walianza kujaa katika lile eneo,  aliyenivunja shingo akakimbia, lakini nikamshika shati  yule wa mbele aliyenipiga na chuma,” anasema

Katika kujaribu kukimbia, kijana aliyeshikwa shati alimng’ata Mishaly mdomoni. Alimng’ata kwa nguvu kiasi kwamba meno yalipenyeza ndani ya mdomo.

Baada ya kumng’ata alivua shati lake na kukimbilia katika vichaka.

Mishaly alipelekwa polisi na wasamaria wema, hata hivyo ilimchukua saa nne kuandikiwa PF3, na aliendelea kuteseka na maumivu makali.

“Nilikimbizwa katika hospitali ya Tumbi, lakini hali iliendelea kuwa mbaya na nikapewa rufaa ya kwenda Muhimbili. Hata hivyo nilikutana na mgomo mkali wa madaktari,” anasema

 Ilimchukua muda kupata huduma stahiki, na akiwa hapo Muhimbili, mwili wake wote ukaingia ganzi.

 “Sikuwa na hisia zozote kuanzia mikononi hadi miguuni…sikuweza kufanya chochote, kichwa changu tu ndicho kilikuwa na ufahamu” anasema
Alihamishwa tena na kupelekwa katika hospitali ya Dk Bakes ambapo ndipo kazini kwake. Hapo Mishaly alipata matibabu mazuri, anakiri kuwa mwajiri wake alitumia ujuzi wake kumtibu pale alipoweza.

Picha ya X-ray ilionyesha kuwa pingili tatu za uti wa mgongo wa Mishaly zimekatika. Lakini pia, nyonga yake ilikuwa imeharibiwa vibaya.

 Aidha, shingo yake lilikuwa limeharibiwa na kuvunjika vunjika.

“Nilitakiwa kwenda Muhimbili kwa wataalamu wa mishipa lakini hata hivyo wakasema hawataweza kunifanyia upasuaji kwa sababu mishipa yangu ya damu imekufa. Wanachoweza kunisaidia ni mazoezi tu,” anasema

Mishaly anatakiwa kufanyiwa upasuaji nchini India, ili arejee tena katika uzima wake wa awali.

Akiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto tisa, Mishaly hana ndugu hapa jijini na hivi sasa amepewa hifadhi katika familia ya mzee wa kanisa lake.

“Familia yangu ni ya kimaskini, mama yangu ni mgonjwa yu taabani, na sijui nitapata wapi fedha za kutibiwa nje ya nchi,” anasema

 Hata fedha za kwenda kufanya mazoezi Muhimbili, Mishaly huchangiwa na waumini wenzake.

 Mishaly, binti mdogo ambaye bado mchango wake unahitajika kwa taifa, hajiwezi kwa lolote. Ni wa kubebwa, kufuliwa, na muda wake mwingi anautumia akiwa kitandani.

 Baada ya mazungumzo yetu, Mishaly anamaliza na ujumbe huu:

“Namuomba Mungu aninyanyue hapa kitandani, na iwapo haitampendeza mimi kunyanyuka, basi …namsihi niwepo katika ufalme wake”.

Familia ya Mzee Nyange inayomtunza Mishaly haikutaka kuzungumza lolote.